Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Author "Nassor Ali, Yakuti"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
- ItemTathmini ya Utoaji wa Maelezo ya Utamaduni katika Kufundisha Kiswahili kama Lugha ya Kigeni(SUZA, 2019-12-01) Nassor Ali, YakutiUtafiti huu umeshughulikia; Tathmini ya Utoaji wa Maelezo ya Utamaduni katika Kufundisha Kiswahili kama Lugha ya Kigeni. Maelezo ya utamaduni ni kipengele muhimu sana katika ufundishaji wa lugha. Maelezo hayo yamebainishwa kwa ufupi katika vitabu kulingana na mada husika. Mwalimu amepewa nafasi ya kutoa maelezo ya ziada kuhusu utamaduni kwa kutumia mbinu mbalimbali. Utafiti umefanywa Unguja, Mkoa wa Mjini Magharibi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Taasisi ya Kiswahili na Utamaduni (KIU). Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kubainisha maelezo ya utamaduni yanayotolewa katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, kutathmini mbinu anazotumia mwalimu kutoa maelezo ya utamaduni katika kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni na kueleza umuhimu wa maelezo ya utamaduni katika kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni. Jumla ya watoa taarifa tisa (9) walihusiswa kutoa taarifa katika utafiti huu. Watoa taarifa hao ni walimu wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni ambao walichaguliwa kwa kutumia sampuli lengwa kulingana na upatikanaji wao. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano, ushuhudiaji na uchambuzi ws nyaraka. Utafiti uliongozwa na nadharia ya utamaduni jamii iliyotumika kuangalia maelezo ya utamaduni kama kitu kipya na muhimu anachotakiwa kupewa mwanafunzi katika ufundishaji lugha na mbinu za utoaji wa maelezo ya utamaduni katika kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti ulitathmini na kushughulikia utoaji wa maelezo ya utamaduni kwa wanafunzi wa kiwango cha kwanza. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa: walimu wanatumia mbinu mbalimbali kutoa maelezo ya utamaduni lakini mbinu zinazotumika haziwasaidii sana walimu kufundisha wanafunzi wa kiwango cha kwanza kwa urahisi zaidi. Utafiti umependekeza walimu wapewe mafunzo ya kutosha kuhusu utoaji wa maelezo ya utamaduni na matumizi ya mbinu ya teknolojia katika utoaji wa maelezo ya utamaduni kama vile televisheni na mkazo zaidi utolewe kwa walimu wanaofundisha wanafunzi wa kiwango cha kwanza.