Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Author "Hamad Saleh, Fatma"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
- ItemChangamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni katika Darasa Mseto la Wingilugha(SUZA, 2019-12-01) Hamad Saleh, FatmaUtafiti huu ulichunguza changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika darasa mseto la wingilugha. Ulibainisha changamoto za walimu katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika darasa mseto la wingilugha, changamoto za wanafunzi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika darasa mseto la wingilugha na kufafanua namna walimu wanavyokabiliana na changamoto katika kufundisha na wanafunzi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika darasa mseto la wingilugha. Utafiti huu ulitumia nadharia ya viwezeshi katika masomo ya wingilugha. Utafiti huu ulifanyika Zanzibar, katika kisiwa cha Unguja. Data zilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Watoa taarifa wa utafiti huu ni walimu waliotoka katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni chuoni hapo. Data za msingi zilikusanywa kwa njia ya usaili na ushuhudiaji na katika uchambuzi wake ulitumika mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa walimu wanapata changamoto katika kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika darasa mseto la wingilugha. Miongoni mwao ni walimu kukosa ujuzi wa kutosha wa ufundishaji wa darasa kama hili, ugumu wa kutafsiri wanapokuwa wanafundisha na kulazimika kuchanganya lugha, tafauti za kitamaduni, na nyinginezo. Utafiti ulibaini kuwa wanafunzi wanapata changamoto za tafauti za kiutamaduni, hadhi zao, athari ya lugha ya kwanza katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Utafiti ulipendekeza kuwa; walimu wapatiwe mafunzo ya kutosha katika kufundisha Kiswahili kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni hasa darasa mseto la wingilugha, walimu wajifunze lugha nyengine za kigeni pamoja na utamaduni wake. Vilevile wawe na ubunifu wa kutumia mbinu na viwezeshi muafaka pamoja na zana za kisasa kwa madarasa kama haya. Kwa upande wa wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili darasani, kuheshimu utamaduni wa kila mwanafunzi, kutotilia maanani tafauti ya mwanafunzi mmoja na mwengine na nyenginezo.