TATHMINI YA MITINDO BINAFSI INAYOTUMIWA NA WANAFUNZI KATIKA KUJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI

No Thumbnail Available
Date
2022-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulitathmini mitindo binafsi inayotumiwa na wanafunzi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti ulikuwa na malengo mahsudi matatu; ambapo lengo la kwanza, lilikuwa kubainisha mitindo binafsi ya wanafunzi katika kujifunza Kiswahili. Lengo la pili lilihusu kufafanua kiwango cha matokeo chanya ya mitindo binafsi ya wanafunzi katika kujifunza Kiswahili, na lengo la tatu lilihusu kutathmini kiwango cha matokeo hasi ya mitindo binafsi. Data za utafiti zilikusanywa uwandani na maktaba kwa kutumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data kama vile usaili na hojaji ambapo data za maktaba zilipatikana kwa upitiaji wa maandiko. Mkabala wa maelezo ulitumika katika uchambuzi wa data ambapo programu ya SPSSilitumika kupata takwimu za majadweli, michoro na magrafu ambayoyamefanunuliwakwa maelezo.Nadharia ya Vipawa Mseto “Multiple Inteligence Theory”ilitumika kuongoza uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa kuna mitindo tafauti inayotumiwa na wanafunzi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Mitindo hiyo ni kama vile, mtindo wa kuona, kusikia na mtindo wa mazungumzo. Aidha,utafiti umebaini kuwaasilimia 89.5 ya mitindo inayotumiwa na wanafunzi ina kiwango cha matokeo chanya katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Pia, silimia10.5 ya watoataarifa walijibu kuwa mitindo hiyo ina kiwango cha kati. Kwa uapande wa kubainisha kiwango cha matokeo hasi, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwawatoataarifa 20 sawa na asilimia 100 walieleza kuwa mitindo hiyo haina matokeo hasi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya Kigeni. Mwisho utafiti huu umehitimisha kuwa iwekwe mkakati maalumu wa kutumia marafiki wa lugha katika kuwasaidia wanafunzi kujifunza lugha kwa urahisi na wepesi. Vilevile,utafiti unatoa mapendekezo kwa watafiti wengine kuwa wafanye tafiti zaidi kuhusu mitindo ya kufundishia Kiswahili kama lugha ya kigeni.
Description
Utafiti ulikuwa na malengo mahsudi matatu; ambapo lengo la kwanza, lilikuwa kubainisha mitindo binafsi ya wanafunzi katika kujifunza Kiswahili. Lengo la pili lilihusu kufafanua kiwango cha matokeo chanya ya mitindo binafsi ya wanafunzi katika kujifunza Kiswahili, na lengo la tatu lilihusu kutathmini kiwango cha matokeo hasi ya mitindo binafsi. Data za utafiti zilikusanywa uwandani na maktaba kwa kutumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data kama vile usaili na hojaji ambapo data za maktaba zilipatikana kwa upitiaji wa maandiko. Mkabala wa maelezo ulitumika katika uchambuzi wa data ambapo programu ya SPSSilitumika kupata takwimu za majadweli, michoro na magrafu ambayoyamefanunuliwakwa maelezo.
Keywords
Citation