Tathmini ya Ziada za Kimasoma katika Ufundishaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni: Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar

No Thumbnail Available
Date
2019-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu tathmini ya ziara za kimasomo katika ufundishaji wa Kiswahilili kama lugha ya kigeni; Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Ziara zilizochunguzwa ni ziara za kimasomo zinazoendeshwa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Utafiti ulifanywa katika wilaya ya mjini Unguja, Zanzibar katika Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Data zilipatikana kwa njia ya usaili na ushuhudiaji. Watoa taarifa walikuwa ni walimu wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni SUZA pamoja na wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni chuoni hapo. Mbinu zilizotumika zilisaidia kupata data za kutosha ambazo baadae zilichambuliwa kwa njia ya maelezo na kukamilisha malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kubainisha hatua za kitaaluma zinazofuatwa katika kuwaandaa wanafunzi kwenda katika ziara za kimasomo katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, kuchambua mambo wanayofanya wanafunzi wakati wa ziara za kimasomo katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni na kutathmini ni kwa namna gani ziara za kimasomo zinawasaidia wanafunzi katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Mtafiti alisoma kazi tangulizi mbalimbali na zilimsaidia kupata mwanga wa kufanya kazi yake kwa kujua mambo mbalimbali yaliyoandikwa awali kuhusiana na ziara za kimasomo. Nadharia jamii katika kujifunza ilitumika kukusanya na kuchambua data zilizopatikana katika kazi hii. Utafiti umedhihirisha kuwa kuna hatua kadhaa zinazofuatwa katika kuwaandaa wanafunzi kwenda katika ziara za kimasomo katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni ambazo zinasaidia idara kudhibiti vyema ziara hizo. Hatua hizo ni kutoa ratiba ya siku ya ziara, kutoa mwongozo wa ziara na kuwapa wanafunzi maswali yanayohusu ziara watakayokwenda.
Description
Utafiti huu unahusu tathmini ya ziara za kimasomo katika ufundishaji wa Kiswahilili kama lugha ya kigeni; Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Ziara zilizochunguzwa ni ziara za kimasomo zinazoendeshwa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Utafiti ulifanywa katika wilaya ya mjini Unguja, Zanzibar katika Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar
Keywords
Tathmini ya Ziada za Kimasoma katika Ufundishaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni
Citation