Browsing by Author "MOHAMED,Khadija Tahir"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
- ItemUCHESHI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KWA WAGENI:(SUZA, 2021-12-01) MOHAMED,Khadija TahirUtafiti huu unahusu Ucheshi katika Ufundishaji wa Kiswahili kwa Wageni ambao umeangazia zaidi katika matumizi ya katuni katika stadi ya mazungumzo. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya katuni kama sehemu ya ucheshi wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Malengo mahasusi yalikuwa ni kubainisha aina za katuni zinazotumika katika kufundishia Kiswahili kwa wageni, kuchambua athari zinazotokana na matumizi ya ushechi wa katuni wakati wa kufundisha, kuchambua mbinu zinazotumika kuwasilisha maudhui kupitia katuni darasani na kutathmini mitazamo ya wanafunzi kwenye matumizi ya ucheshi wa katuni katika ufundishaji.Utafiti uliongozwa na nadharia za Ucheshi (Theory of Humours) pamoja na nadharia yamodeli ya ufuatilizi (Monitor Model). Utafiti umetumia mkabala wa kimaelezo naumefanywa ndani ya wilaya ya Mjini katika mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar. Walengwa wa jumla walikuwa ni walimu wenye uzoefu kuanzia miaka mitatu na kuendelea ambao walichaguliwa kwa mtindo wa usampulishaji nasibu. Sampuli ilikuwa ni walimu watano (5) waliokuwa na wanafunzi kipindi ambacho data zinakusanywa. Aidha utafiti umetumia mbinu ya uchunguzi, usaili na uchambuzi wa nyaraka ili kupata data zenye kuaminika. Uchunguzi ulifanyika ndani ya Idara ya Kiswahili kwa Wageni ya Chuo Kikuu cha Zanzibar. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwepo kwa aina mbili za katuni zinazotumika katika ufundishaji wa Kiswahili katika chuo cha SUZA (katuni mjongeo na katuni tuli). Aidha ucheshi katika katuni umeonesha athari kubwa kwa wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni na athari hizo zimegawanywa katika aina mbili athari chanya na athari hasi, kwa upande wa thari chanya ni kujenga misamiati na kupata mitindo ya lugha, kutambulisha utamaduni wa lugha na kuongeza kujiamini kwa wanafunzi, kwa upande wa athari hasi ni muda kuwa mchache na uteuzi wa katuni kuwa mgumu. Mitazamo ya wanafunzi inaashiria kwamba utumiaji wa ucheshi wa katuni katika kufundishia stadi ya mazungumzo huwafanya kufurahia somo na kuvutika nalo na zaidi ya hayo ni kuwapatia kumbukumbu ya muda mrefu ya jambo lililofundishwa darasani. Kulingana na matokeo yaliyopatikana, mtafitialipendekeza kwa Idara ya Kiswahili kwa wageni (SUZA) kushirikiana na wadau mbalimbali wa taaluma na wadau wa maendeleo, kuandaa katuni mahususi kwa ajili ya kufundishia stadi mbali mbali za lugha na sarufi kwa ujumla kupitia usaidizi wa teknolojia. Mapendekezo hayo ni kufuatia kuibuka kwa teknolojia nyingi ambazo zinaweza kutumiwa ili kuendana na ufundishaji wa lugha kimataifa