• Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  • Researches
  • SUZA Repository
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "ALI,Maryam Kombo"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    MATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA
    (SUZA, 2022-12-01) ALI,Maryam Kombo
    Utafiti huu unahusu matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi „B‟ Kisiwani Unguja na kuhusisha kampuni ya Progressive Marketing Company Limited na Sumbezi Marketing Directing. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Jumla ya watoataarifa 29 walihusishwa katika utafiti huu. Mazungumzo kumi (10) ya kimaandishi yalichanganuliwa ili kupata data ya mikakati ya upole kukidhi lengo la kwanza. Data hiyo ilipatikana kupitia mbinu ya ushuhudiaji, hata hivyo mbinu ya mahojiano ilitumika kupata maoni yaliyolikamilisha lengo la pili. Hatimaye uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo.Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987). Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wauza bidhaa za promosheni majumbani hutumia mikakati minne ya upole yaani; mkakati wa kuzungumza kwa uwazi, mkakati wa upole chanya, mkakati wa upole hasi na mkakati wa kuzungumza kwa kuficha katika mazungumzo yao wakati wanapoamiliana na wateja wao. Halikadhalika kupitia data ya maoni, wasailiwa walikiri kuwa matumizi ya lugha ya upole husaidia kujenga heshima, kukuza mahusiano mazuri baina ya wauzaji na wanunuzi na kuongeza mauzo katika biashara yao. Kwa ujumla, utafiti unapendekeza kufanyika kwa tafiti zaidi zitakazobainisha vipengele vya kilughawiya vinavyounda lugha ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.

Contacts

  • Director of library Service.
  • P.O BOX 146, Zanzibar
  • library@suza.ac.tz
  • suza.ac.tz
  • Main Campus.
  • Tunguu, Zanzibar, Tanzania

Other Resources

  • Open Access Policy
  • Open Data
  • Term of Use
  • Frequently asked questions (FAQ)

The State University of Zanzibar. © 2025.

  • Cookie settings
  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback